Thursday, July 26, 2007

Cultural Heritage in Zanzibar



Hili jengo linaitwa Old Dispensary, likiwa limesimama imara ndani ya Mji Mkongwe Unguja.Kitu hicho ni cha zamani wapendwa! miaka ya 1887. Lilitumika kama dispensary katika ground floor na makazi kwa upande wa ghorofa. Baada ya kukimbiwa na wenyeji wake yalipotokea Mapinduzi 1964, jengo likawa katika mikono ya serikali.

Mwaka 1997 jengo likafanyiwa ukarabati (restoration) na Aga Khan Trust for Culture na kuzinduliwa na Dr.Salmin Amour akiwepo pia Prince Karim Aga Khan.

Hivyo hili jengo ni moja ya majengo mengi ya Stone Town Zanzibar yaliyofanyiwa restoration na hiyo taasisi.

Jengo limetulia humo ndani si mchezo! Matunda ya human imagination bila shaka. Kudadadadeki!!

Moses.a.k.a MwanaHekima.

Zanzibar.

No comments: